Jina la Mwigizaji Steve Nyerere limerudi kwenye headlines kwenye mitandao ya kijamii hii ni baada ya kupokea jumbe za utani za baadhi ya mashabiki kuhusiana na kifo cha Ibrahim Pasha kupitia tamthiliya ya Sultan inayooneshwa na Azam TV.
Kupitia caption aliyoiandika Steve Nyerere kwenye ukurasa wa instagram unaonyesha kuwa mashabiki wamemtaka aanzishe mchango kutokana na wengi kudai kuwa Misiba mingi ya wasanii, Steve huwa anakuwa katika mstari wa mbele wakidai kuhamasisha upatikanaji wa michango.
Pasha amefariki lakini kufariki kwa Pasha ni katika tamthilia ya Sultan, hivyo Steve ameamua kuwajibu wale wanaomtania kuwa aanze utaratibu wa kuratibu mazishi ya Pasha “Nimeona sms zenu kuhusu ibrahim pasha , Nimebaki nacheka TU mitandao hiii DOOO, Aya jibu lenu ni hili Wasaniii Wote tukutane lidas fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuu Ila niacheni KIDOGO nipumue kaaaaaaaa ππππππππππππ”