Ikiwa zimepita siku 5 tokea Rapper Cardi B atangaze rasmi kuachana na Mume wake Offset kupitia page yake ya Instagram inaonekana kuwa Offset bado ana mkumbuka baby mama wake Cardi B hii ni baada ya ujumbe aliouandika kupitia mtandao wa Twitter.
Lakini Jumamosi ya December 8,2018 Cardi B alipopanda kwenye stage Chicago alioonekana kumuongelea vibaya Offset kwenye baadhi ya mistari kwenye ngoma yake ya ‘Motorsports’ na kusema ‘kuna siku nilimwambia kuwa tutapeana talaka’.
Vyanzo vya karibu na Offset vinaripoti kuwa rapper huyo alijaribu kuweka sawa ndoa yake kabla ya Cardi B kuweka wazi kuwa wameachana lakini ishu hiyo ilionekana ku-fail hii ni baada ya mashabiki kuandika vitu vibaya kuhusiana na Offset kwenye mitandao ya kijamii.
Sababu ya wawili hao kuachana inatajwa kuwa Offset alipanga kujihusisha kufanya mapenzi ya watu watatu na mwanadada aliyefahamika kwa jina la Summer Bunni pamoja na rafiki wa Summer. Kupitia mtandao wa TMZ uliripoti kuwa mwanadada huyo ameomba radhi akihisi amehusika kuvunja ndoa ya Offset na Cardi B
VIPAJI MTAANI: Ametoka Mtwara, Kaingia DSM msikilize anavyoimba kikongo