Kampuni ya Ndege ya Precision Air imethibitisha kwamba Ndege yake aina ya PW 722 iliyokuwa ikitoka Nairobi kupitia Kilimanjaro kuelekea Mwanza iligongana na kundi la Ndege wakati ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Kampuni hiyo imeeleza kwamba kwa ujuzi, umaridadi na juhudi za Marubani wa ndege hiyo walifanikisha zoezi la kutua kwa ndege hiyo kwa usalama kabisa bila kusababisha madhara yeyote kwa Abiria 68 na Wafanyakazi wanne waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Inaelezwa kitendo cha kundi la ndege kugongana na Ndege angani ni cha hatari sana na kinahitaji Marubani kujiamini na kuwa makini sana ili Ndege isianguke.
Aidha kwa sasa Ndege hiyo ipo chini ya Wataalamu wakiichunguza kubaini madhara yaliyojitokeza kutokana na mkasa huo na hatua za kuchuuka kukabiliana na madhara yatakayokuwa yamejitokeza.
Pia Precision Air imewashauri Abiria wote walioathirika kutokana na mkasa huo kubadilisha Ndege zao na imewaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
HUYU NDIE SULTAN SULEIMAN WA TAMTHILIA YA SULTAN 👑, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA