Muigizaji wa Hollywood Gabrielle Union pamoja na mume wake Dwyane Wade wameelezea safari waliopitia mpaka kubahatika kumpata mtoto wao wa kwanza pamoja November 7,2018 ikiwa na furaha walionayo baada ya mtoto huyo kuja kwenye maisha yao.
Gabrielle Union pamoja na Mumewe walitumia njia nyingi kupata mtoto pamoja lakini ilishindikana ambapo Muigizaji huyo hakukaa tamaa baada ya mimba zaidi ya tisa kuharibika (miscarriage) na kugundulika kuwa alisumbuliwa na ugonjwa wa Endometriosis ambao ulimzuia kupata ujauzito.
Gabrielle Union aliamua kuandika ugumu aliopitia katika maisha yake kupitia kitabu chake cha ”We’re Going to Need More Wine” ikiwa mtoto huyo alipatikana kwa njia ya surrogate (Mama Mbadala).
EXCLUSIVE: HAMISA AMEJIBU KWENDA DUKANI KWA WEMA NA KUHUSU OFFICIAL LYYN