Siku moja baada ya kiungo wa zamani wa Man City raia wa Ivory Coast Yaya Toure atangaze kuvunja mkataba na club ya Olympiakos ya Ugiriki, leo amesafiri kutoka Ugiriki kuelekea London England kwa ajili ya kwenda kutafuta Club ya muda ya kufanya nayo mazoezi wakati huu akitafuta timu mpya.
Toure msimu huu amecheza game 5 akiwa na Olympiakos ya Ugiriki ambayo alijiunga nayo na kudumu nayo kwa miezi mitatu, hata hivyo mkataba wa Toure na Olympiakos ambao haukuwahi kuwekwa hadharani ulidumu kwa miezi mitatu pekee.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Yaya Toure alidumu na Man City kwa miaka nane toka alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea club ya FC Barcelona ya Hispania ambayo nayo alidumu nayo kwa miaka mitatu pekee, hiyo ni baada ya kutoka AS Monaco ya Ufaransa.
Inaripotiwa kuwa wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk amekuwa katika mazungumzo na Crystal Palace na West Ham United kwa ajili ya mteja wake ajiunge navyo, Toure amekataa ofa ya kwenda kucheza soka China na Marekani kufuatia kuonesha dhamira yake ya kutaka kucheza Ligi Kuu England.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe