Watu wanne wamepoteza maisha katika matukio mbalimbali wakati wakisheherekea Sikukuu ya Krismasi katika Mkoa wa Kagera jambo ambalo limezua taharuki Mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amewataja watu hao waliopoteza maisha na sababu zilizopelekea vifo hivyo huku akiwaomba Viongozi wa Dini kuhubiri amani ili wananchi wawe na hofu ya Mungu.