Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amezungumzia suala la majungu katika ofisi mbalimbali huku akiwatahadharisha Katibu na Naibu Katibu wa wizara hiyo walioteuliwa hivi karibuni kujiepusha na mambo hayo na kuwataka wachukue hatua.
Jafo amesema matamanio yake ni kuhakikisha wizara hiyo inakuwa bora zaidi kwani historia ilipotoka hasa wakati Rais John Magufuli alipolihutubia Bunge November 20, 2015 aliitaja wizara ya TAMISEMI kwa sababu ilikuwa miradi yake inatekelezwa hovyo.
“Kipindi hicho ilikuwa ukiitafuta TAMISEMI katika kumi bora haipo, lakini sasa hivi huwezi kuikosa TAMISEMI katika tatu bora,”
Pia amesema sehemu yoyote majungu yapo, licha ya kuwa TAMISEMI hakuna lakini anawahasa viongozi hao wapya kulifanyika kazi suala hilo.
“Mara nyingiviongozi wapya wanapokuja ndio majungu yanaanza, mnapigwa dozi CC 10 za kutiosha jkwani unaanz akuchukia watu hataka bado hujaanza kufanya nao kazi,”amesema.