Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema vitisho vinavyotolewa na baadhi ya Wasanii dhidi ya watendaji wanaowachukulia hatua za kisheria haviwezi kuwafanya watendaji hao waache kusimamia sheria za nchi.
Ameyasema hayo Mkoani Mbeya alipokuwa anazungumza na AyoTV kuhusu usimamizi wa maadili ya Wasanii ambapo alisema yeye katika utendaji wake hajakutana na vitisho vya aina yoyote.
Amewataka wasanii kufuata Sheria za Nchi wanapofanya sanaa zao pamoja na kufuata misingi iliyowekwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kuepuka kuingia kwenye migogoro na Serikali.
RC MBEYA “KIAMA WALIOTAFUNA FEDHA ZA AIRPORT CHAJA, JPM KAGOMA KUTOA BILIONI 18”