Mtandao wa dailymail.co.uk umeripoti kuwa kocha mkuu wa muda wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameamua kurudisha utaratibu wa zamani wa wachezaji wa Man United kwenda uwanjani siku ya mechi wakiwa wamevaa suti kama ilivyokuwa kwa kocha wa zamani wa timu hiyo.
Enzi za kocha Sir Alex Ferguson wachezaji wa Man United walikuwa wanavaa suti za club wakati wakielekea uwanjani kucheza mechi lakini baada ya kustaafu Ferguson mwaka 2013, wachezaji hao walikuwa wakiingia uwanjani wakiwa wamevaa tracksuit utaratibu ambao, Ole Gunnar ameamua kuufuta na kurudisha wa zamani.
Ole Gunnar Solskjaer ameripotiwa kuwaagiza wachezaji wake kuwa muonekano nadhifu ni sehemu ya sheria zake za uwanjani, japo wachezaji hao wanaruhusiwa kuvaa tracksuits wakati wa safari ila wanapokuwa wanaelekea uwanjani wote wanatakiwa kuvaa suti rasmi za club hiyo, huo ni utaratibu wa zamani wa kocha Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kuifundisha timu hiyo baada ya kudumu kwa miaka 27.
Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake