Moja kati ya habari kubwa katika tasnia ya michezo iliyoripotiwa leo Jan 17 ni kuuawa kwa Mwandishi wa habari za uchunguzi Ahmed Hussein-Suale kwa kupigwa risasi tatu na Watu wasiojulikana wakati akitoka katika mizunguko yake akirudi nyumbani.
Ahmed ambaye amepigwa risasi tatu na Watu waliokuwa katika pikipiki, yeye akiwa kwenye gari lake, alikuwa ndio Mwandishi aliyefanya habari za uchunguzi wa sakata la rushwa katika Shirikisho la Soka nchini Ghana uliopelekea kujiuzulu kwa Rais wa Shirikisho hilo.
Mwandishi huyo aligundua mambo mengi ya rushwa katika michezo ikiwemo hilo la Ghana na lile la Kenya ambapo Muamuzi mmoja wa nchi hiyo aliondolewa katika Waamuzi waliokuwa wamepangwa kuchezesha Kombe la Dunia mwaka 2018 baada ya uchunguzi wake kumbaini kwamba alipokea rushwa.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”