Baadaa ya mapumziko ya Siku Kuu ni muda Ligi Kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga, kuelekea kumaliza mzunguuko wa kwanza na kuanza mzunguuko wa pili ama hatua ya lala salama ni nafasi kwa timu zilizofanya vibaya mzunguko wa kwanza kupindua matokeo, na kwa zile zilizofanya vizuri kuendelea kujiimarisha zaidi.
Leo Bayern Munich ambao hawakufanya vizuri sana mzunguko wa kwanza wana nafasi ya kusahihisha makosa na kuanza kuwafukuzia Borussia Dortmund wanaoongoza ligi kwa sasa kwa tofauti ya point 6 dhidi yao. Bayern Munich watakuwa ugenini kwa Hoffeiheim kwenye mchezo utakaopigwa saa 4:30 Usiku majira ya Afrika Mashariki ila wanaweza kukutana na ugumu kutokana na Hoffenheim kutoka sare game 5 zilizopita za Bundesliga hivyo wanatajwa kuwa vizuri kwa kujihami ila Bayern wanaweza kufanya kitu kutoka na kushinda game 5 mfululizo.
Mchezo mkubwa wikendi hii unatarajiwa kuwa ule wa RB Leipzig dhidi ya vinara Borussia Dortmund. Leipzig watakuwa nyumbani katika dimba la Red Bull Arena kukabiliana Dortmund wamepoteza mchezo mmoja tu hadi sasa. Mechi hiyo itachezwa siku ya Jumamosi saa 2:30 na RB Leipzig wanatajwa kuwa wataleta ushindani.
Kocha wa Dortmund Lucian Fevre huenda anasema nyota wake Marco Reus na kinara wa magoli Bundesliga Paco Alcacer wako fiti kucheza mchezo wa Jumamosi. Reus alikuwa anasumbuliwa na tumbo, huku Alcacer akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Kwa upande wa RB Leipzig wao wako vizuri na watawategemea zaidi Timo Werner mwenye kasi zaidi na Mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen ambaye ana nguvu kuwasumbua mabeki wa kati wa Dortmund Dani Axel Zagadou na Manuel Akanji, game hizo zitaoneshwa na Star Times
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”