Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye vitu vya kale ambavyo havipatikani sehemu yeyote Duniani, moja kati ya vitu hivyo ni Kinyago cha Makonde ‘Handsome Boy’ kilichonakishiwa kwa nywele halisi za Binadamu kwa kutumia mkojo wa Pimbi.
Afisa wa Sheria Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Caroline Joseph amesema kinyago hicho kiliibiwa kutoka Makumbusho ya Taifa ya Tanzania mwaka 1980 na kukutwa katika Makumbusho ya Uswisi.
Kutokana na hatua hiyo, amesema Makumbusho ya Tanzania ilifanya mchakato wa kukirudisha kinyago hicho ambapo walivutana kwa muda mrefu na Uswisi takribani miaka 30 na kisha wakafanikiwa kukirejesha nchini mwaka 2010.
“Tulirudishiwa kinyago hiki kwa sherehe kubwa mjini Paris, ukikiangalia ni kama burudani lakini kinaonyesha jinsi binadamu walivyo, kwani nilipokifanyia utafiti niligundua kina nywele za hasili za Binadamu zilizogandishwa kwa kutumia mkojo wa Pimbi,”amesema.