Leo January 21, 2019 Kampuni ya Foshan Guangji ya nchini China imesema itajenga kiwanda cha kuzalisha wanga kwa kutumia muhogo katika Wilaya ya Handeni.
Akizungumza na AyoTV na millardayo.com Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe amesema kiwanda hicho kinatarajiwa kumaliza tatizo la kuharibika kwa muhogo ambao Wananchi wameulima kwa nguvu kubwa kwa miaka mitatu ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano.
JAMAA ATELEKEZA GARI BAADA YA KUTOA RUSHWA LAKI TANO