Baraza la Mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na TANESCO kwa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) na kufuta malimbikizo ya deni la kodi ya VAT lililofikia Bilioni 22.9 kwa TANESCO kwenye umeme uliouzwa ZECO.
Baraza la Mawaziri limefanya uamuzi huo leo katika kikao kilichoongozwa na Rais Magufuli na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Mawaziri.
“Kwa hiyo madeni yatakayokuwa yanadaiwa kwa Zanzibar ni yale madeni ya kulipia umeme, umeme wametumia kiasi fulani wanalipa kama wanavyolipa wa maeneo mengine kwa mfano wanavyolipa DSM, suala la kutoza VAT sasa halipo” JPM
“Katika hilo kwa sababu kulikuwa na deni ambalo lilikuwa limefika Bilioni 22.9, sisi Baraza la Mawaziri tutapeleka mapendekezo Bungeni kwamba lisamehewe kwa sababu lipo ndani ya bajeti ya mwaka huu wa 2018/19, kwa hivyo litapunguza mapato yatakayotakiwa kukusanywa na Serikali” JPM
KILICHOTOKEA BAADA YA CAG KUHOJIWA BUNGENI, VIPI HALIMA MDEE?