Wananchi wa Kata ya Muhange wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma wamepongeza ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, kwa kuamua kujenga soko la pamoja la mpakani ambalo wameeleza kuwa litawaletea manufaa makubwa ya kiuchumi.
Katika mradi wa soko hilo Serikali ya Tanzania ilitenga Milioni 178.6 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019, huku Serikali ya Norway kupitia shirika la UNCDF ambalo ni moja kati ya Mashirika 16 ya umoja wa Mataifa yanayotekeleza program ya pamoja ya Kigoma, wakitoa Milioni 270.3.
EXCLUSIVE: DC Gondwe afunguka “Siku nateuliwa nilishakula hela za U-MC, Eminem anatukana”