Kupitia mahojiano aliyoyafanya Darasa leo January 25,2018 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM amefunguka kuhusu ishu ya ukimya wake wa mwaka mmoja ikiwemo tuhuma zilizokuwa zikiendelea mtaani juu yake baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye game ya Bongo Fleva.
Hivi ndio vitu vinne vya msingi alivyoviongea Darasa.
“USHINDANI UTAKUWA MKUBWA” @officialdarasa “Mtoto wangu ana mwaka na miezi sita, siwezi kuoa kimya kimya kwani hata mtu ambaye nimezaa nae tupo kwenye mahusiano miaka nane” .
“Nimekaa ndani kwa mwaka mzima, Wasanii wengi wametoa ngoma zao na zimefanya vizuri, natumia fursa hii kumpongeza producer @abbah_process kwa kufanya ngoma nzuri ya #Iokote, Watu wajue nimeanza kazi rasmi na ushindani utakuwa mkubwa”
“Ni kweli nilikaa kimya sababu nilikuwa nimepata mtoto na muda wangu mwingi nilikuwa nautumia nikiwa nyumbani na hata hizo story ambazo zilikuwa zinaendelea juu yangu nilikuwa nazisikia nikiwa nyumbani kwangu huku nikiwa nimembeba mtoto wangu, Ilifika time watu walikuwa wanakuja kugonga nyumbani kwangu ili wanione je ni kweli yanayoendelea na ikawa inafika muda nafungua geti na nawauliza vipi mnaona nini”
“Unaanzaje kujiogopa mwenyewe, siwezi nikasema hiyo ndiyo sababu ambayo ilinifanya nikae kimya maana siwezi nikakosa usingizi sababu ya darasa juu ya darasa”
MPENZI MPYA WA HAMISA AMTOA CHAMBO CARRY “DOGO TOA HIYO KABLA SIJAKUZAA MTOTO WA PILI”