Hadi sasa matumaini ya watu na wapenzi wa soka duniani kupata taarifa za wapi alipo Emiliano Sala wa Cardiff City pamoja na rubani wake David Ibbston waliyepotea nae kwenye ndege ndogo binafsi wakitokea Nantes nchini Ufaransa yanazidi kukatika ya kuwapata wakiwa hai.
Baada ya Polisi na kikosi kazi cha uokoaji kutangaza wamesitisha zoezi la kumtafuta Emiliano Sala na rubani wake baada ya kuwatafuta kwa saa 80, watu zaidi ya 4000 ikiwemo mastaa wa soka wamekusanya zaidi ya euro 300000 ambazo ni zaidi ya Tsh 788 kwa ajili ya kuanza zoezi binafsi la uokoaji.
Inaelezwa kuwa tayari zoezo la utafutaji wa ndege hiyo chini ya bahari unaanza weekend hii kufuatia michango iliyochangishwa huku matumaini ya kuwapata wakiwa hai yakiwa yamepotea, zoezi hilo linatajwa kuanza Jumapili lakini kwa nguvu ya michango ya watu mbalimbali baada ya awali kusitishwa na Polisi kwa kukata tamaa.
Emiliano Sala alijiunga na Cardiff City ya Wales weekend iliyopita kwa dau la pauni milioni 15 akitokea Nantes FC ya Ufaransa na baada ya hapo kurejea Nantes kwa ajili ya kuwaaga wachezaji wenzake na January 21 ndipo akaanza safari ya kurejea Cardiff kuanza maisha mapya ndio ndege yao ikapotea kwenye rada wakiwa pwani ya Guenmay.
Hata hivyo kabla ya ndege kupaa Emiliano Sala alieleza hofu yake ya ndege hiyo na kuwaambia wachezaji wenzake ikipita saa 1:30 hajajibu chochote watume mtu akamtafute
Haji Manara katolea ufafanuzi tuhuma za kuita washabiki wapumbavu