Tunayo story kutokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ambapo ameingilia kati sakata la wavuvi wa Soko la Samaki la Kimataifa Ferry la kukamatwa, kupigwa na kuchukuliwa vifaa vyao vya uvuvi.
Akizungumza na wavuvi wa soko hilo, DC Mjema amesema wizara husika ina wajibu wa kuhakikisha kama kuna wavuvi ambao wanakiuka sheria wapigwe faini na si kupigwa kama inavyofanyika kwa sasa katika oparesheni inayoendelea.
“Hilo nalikemea na tunaendelea kulifatilia ili kuangalia wakina nani wametoa adhabu za kupiga kwani si kazi ya serikali kuwapiga watu, hivyo nalifatilia na hatua zitachukuliwa,”amesema.
Pia DC Mjema amesema analiagiza Jeshi la Polisi kuweka ulinzi katika eneo hilo ili wavuvi wasipigwe na wale wanaokiuka sheria watozwe faini na si kupigwa.