Mzee Jumanne Ngoma ambaye aligundua Madini ya Tanzanite amefariki dunia leo January 30, 2019 katika Hospital ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.
Akithibitisha kifo cha Mzee Ngoma, Mtoto wake ambaye ni Mtangazaji wa Clouds TV Hassan Ngoma amesema Mzee amefariki leo akiwa anapatiwa matibabu na taratibu za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia
Mwaka jana mwezi April, Rais Magufuli na Serikali walitoa Tsh. Milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya Mzee huyo mzalendo.