Mtanzania Shiza Ramadhani Kichuya anayecheza soka la kulipwa nchini Misri katika club ya ENPPI FC kwa mkopo akitokea Pharco FC ya daraja la pili nchini humo, jana February 5 2019 alicheza game yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly.
Kichuya ambaye ndio kajiunga na timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Simba kujiunga na Pharco na kutolewa kwa mkopo ENPPI FC, akiwa uwanjani wameshindwa kuondoka na point wakiwa nyumbani baada ya kuruhusu kufungwa kwa magoli 2-1.
Club ya ENPPI FC inayochezewa na mtanzania Shiza Kichuya kwa sasa imecheza michezo 21 ya Ligi Kuu Misri inayoshirikisha jumla ya timu 16 na baada ya kufungwa kwa magoli 2-1, sasa ipo katika nafasi tatu za chini ambazo ni hatari kwani timu inaweza kushuka daraja.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF