Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ameumwa ghafla akiwa Mkoani Tanga kwenye shughuli za Chama chake cha CHADEMA ambapo yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene imesema amekimbizwa Hospitali ya Bombo na kupatiwa matibabu na inaelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.
“Mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi inafanyika” Mkuu wa Idara ya Mawasiliano CHADEMA Tumaini Makene
WAKIMBIZI WAFURAHI KUMUONA ALIEMUOMBA RADHI RAIS MAGUFULI IKULU