Mitandao ya kijamii imejitokeza na kuendelea kuwa vyombo vya kusambaza habari na taarifa mbalimbali na kwa mifumo mbalimbali. Ili kupata habari na taarifa zilizo sahihi, watumiaji wa mitandao ya jamii wanapaswa kujilinda dhidi ya habari na taarifa za uongo na uzushi.
Watumiaji wanaotegemea mitandao kama vyanzo vya habari au taarifa wanaweza kutambua iwapo
habari na taarifa hizi ni za uongo, uchochezi,uzushi au za kutusi watu wengine. Kuna namna za kugundua iwapo habari ni ya ukweli au la.
3.Chunguza chanzo cha habari: Hakikisha kwamba habari imeandikwa na mwandishi ambaye unamwamini kwamba ana sifa ya kuandika ukweli. Kama habari inatokana na taarifa za taasisi ambayo huifahamu, chukua hatua za kujiridhisha.
4. Angalia usanifu au mpangilio usio wa kawaida: Tovuti nyingi za kughushi zinakuwa na mpangilio
wa maneno na usanifu usio wa kawaida. Kuwa macho ukiona hizi dalili.
5. Angalia vizuri picha: Mara nyingi habari za uongo zinakuwa na picha za kawaida na za video ambazo zimechakachuliwa. Inawezekana picha au video vikawa ni vya kweli lakini vikawekwa kwa mpangilio ambao unaleta maana tofauti na ile ya awali. Ukiona hili tafuta chanzo cha picha ili kuhakikisha ilikotoka.
6. Kagua/chunguza tarehe: Habari za uongo zinaweza kuwa na tarehe ambazo hazina mantiki au hata tarehe ambazo zimebadilishwa.
7. Thibitisha vyanzo vya habari: Chunguza vyanzo vya mwandishi wa habari husika ili kuthibitisha uhakika. Habari ambayo haina maelezo ya kuthibitisha uhalisia wake auinanukuu wahusika ambao hawatajwi ina kila dalili ya kuwa ni ya uongo.
8. Linganisha na taarifa za vyombo vingine: Iwapo hakuna chombo kingine chochote kinachotoa taarifa hiyo, ni dalili kwamba habari hiyo ni ya uongo. Habari inayoandikwa na vyombo vingi ina kila dalili ya kuwa ya kweli.
Namna ya kutambua habari na taarifa za uongo na uzushi mtandaoni