Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeeleza kitaanza kufanya mikutano ya hadhara kwa kile walichokidai kuwa walikuwa wanakabiliwa na mambo mengi ndani ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini DSM Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amesema awali walionekana kutii agizo hilo la katazo ya mikutano ya kisiasa kwa sababu chama hicho kilikuwa kinashughulika na ujenzi wa chama chake.
“Ni kweli tulikuwa na jukumu la ujenzi wa chama kama taasisi, kwa hiyo tulikuwa hatuna uwezo wa kuendesha vitu viwili kwa wakati mmoja.“ Mashinji
“Ndiyo maana wakati tamko linatokea na matendo yetu ilionekana kutii amri isiyokuwa halali bali ni matukio mawili ambayo yaliyotokea kwa wakati mmoja na moja kumeza jingine.” Mashinji.
Waziri Lugola ampa onyo Kamanda “nakunyooshea kidole”