February 16, 2019 Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amefika nyumbani kwa kijana Richard Peter ambaye amefariki siku za hivi karibuni kwa kupigwa risasi akiwa katika kituo cha Polisi Usa River Arusha.
Lugola amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo huku akituma salam za Rais Magufuli nakusema alishtuka baada ya kupata taarifa hizo.
“Alipopata taarifa zilimshtua na sababu moja kubwa ya kumshtua ni kwamba amefia kwenye eneo la Polisi, kwa hiyo amenituma niwapeni pole sana” Waziri Kangi Lugola
EXCLUSIVE:HILI NI GHOROFA LA KWANZA KUJENGWA DAR ES SALAAM “GUEST HOUSE”