Mbunge wa Jimbo la Iramba, Mwigulu Nchemba ameruhusiwa kutoka hospitali kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatano, February 13 mkoani Iringa.
Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao.
“Nashukuru Mungu nimeruhusiwa kutoka Hospitali, shukran kwa Rais na wasaidizi wake wote kwakuwa karibu nami, Wabunge, Viongozi wa Chama na Serikali, Madaktari kwa matibabu ya haraka, wananchi wote kwa maombi yenu na salamu za kunitakia heri” Mwigulu
“Zaidi namshukuru Mungu kwa namna alivyonitetea mimi pamoja na dreva wangu, hakika kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa” Mwigulu
Waziri Lugola afika kaburini kwa aliepigwa risasi na Polisii, atuma ujumbe wa JPM