Michuano ya UEFA Europa League hatua ya 32 bora iliendelea tena Ulaya usiku wa February 21 wakati watanzania wakielekeza macho yao katika mji wa Genk nchini Ubelgiji kuweza kujua nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta atafanya nini akiwa na KRC Genk usiku wa leo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Slavia Praha ya Czech.
Mchezo wa kwanza ambao KRC Genk ulianzia ugenini walitoka sare tasa (0-0) kabla ya leo kuja kucheza game ya marudiano iliyomalizika kwa KRC Genk kupoteza kwa idadi kubwa ya magoli 4-1 wakiwa nyumbani, Genk ambao walikuwa wanaaminiwa kuwa wataitoa timu hiyo kutokana na wao kuwa nyumbani na kutawala mchezo kwa dakika zote 90 wameishiwa kutolewa.
Baadhi ya hoja za wachambuzi wa soka Ubelgiji zinadaiwa kuwa KRC Genk walikuwa na nafasi ya kushinda ila tatizo baada ya Slavia Praha kusawazisha ikawa 1-1 na dakika zinayoyoma ndio wakaanza kupata presha na kuongeza mashambulizi, yaliowapa Slavia Praha nafasi ya kucheza soka kwa kujiamini na kuvuna magoli manne.
KRC Genk ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Leandro Trossard dakika ya 10 lakini yalianza kusawazishwa dakika ya 23 kupitia kwa Coufal na baadae Traore akaongeza goli la pili dakika ya 53, Skoda dakika ya 64 na 64, hivyo Genk ikayaaga mashindano ya UEFA Europa League msimu wa 2018/2019 wakiwa nyumbani kwao.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba