Uongozi wa club ya Chelsea umeamua kuchukua hatua za kinidhamu zaidi kufuatia tukio lililokuwa limejitokeza kati ya golikipa wao Kepa Arrizabalaga kumgomea kocha wake Maurizio Sarri wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la EFL kati ya Chelsea dhidi ya Man City uliyochezwa Jumapili ya February 24 nchini England.
Mchezo huo ambao ulichezwa dakika 120 ilipofika dakika ya 119 Maurizio Sarri alitaka kumtoa golikipa wake Kepa Arrizabalaga na amuingiza Caballero ambaye alikuwa anahisiwa kuwa anataka kwenda kwa ajili ya mikwaju ya penati, ila Kepa aligoma kutoka na hatimae akacheza hadi dakika zote kumalizika na Chelsea ikapoteza kwa mikwaju ya penati 3-4.
Pamoja na kuwa Kepa na Sarri walieleza mbele waandishi wa habari kuwa walishindwa kuelewana kwa madai kuwa kocha alihisi kaumia, ila Chelsea imempiga faini ya kutokumlipa mshahara wake Kepa wa wiki moja wa pound 190,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600, Kepa amekiri kosa na kuomba msamaha kocha, uongozi na wachezaji wenzake.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake