Wafanyabiashara watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ya kuingiza nchini Kemikali bila kuwa na vibali.
Washitakiwa hao ni Jumanne Mazunde, Godfrey Kiwelu, Nsia Mbonika, Chankan Mhina na Joseph Omollo.
Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na wakili wa serikali Wankyo Simon.
Wakili Wankyo amesema washitakiwa wanakabiliwa na makosa manne ya kuingia nchini Kemikali mbalimbali kutokea Nairobi Kenya.
Katika kosa la kwanza linamkabili, mshitakiwa Mazunde ambapo anadaiwa alitenda kosa hilo September 13, 2017 maeneo ya Ubungo ambapo aliingiza nchini Kemikali mbalimbali ikiwemo Potassium Hydrochloride 12.5 Kilogram, Amonium Chloride 99% kutokea Nairobi Kenya.
Pia kosa la pili linamkabili mshtakiwa Mbonika na Mhina ambapo anadaiwa alilitenda September 13, 2017 Ubungo Dar es Salaam ambapo waliingiza Kemikali mbalimbali zikiwemo Potassium Hydrochloride 7.5Kilogram na Sodium Hydrogen Carbonate 29 Kilogram kutokea Nairobi Kenya bila kuwa na vibali.
Kosa jingine linamkabili mshitakiwa Mhina ambapo anadaiwa alitenda kosa hilo September 13, 2017 Ubungo Dar es Salaam ambapo aliingiza Kemikali mbalimbali ikiwemo Polyester resin 100 Kilogram bila kuwa na kibali cha Wizara husika.
Katika shitaka la tano linamkabili mshitakiwa Omollo ambapo anadaiwa alilitenda September 13, 2017 maeneo ya Ubungo ambapo anaidaiwa aliingiza Kemikali hizo kutokea Nairobi Kenya bila kuwa na vibali.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa walikana makosa.Upelelezi wa kesi haujakamilika.
Washitakiwa hao walipewa masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Shilingi Mil. 10 kwa kila mmoja.
Washitakiwa watatu kati ya hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambao ni Kiwelu, Mbonika na Mhina.Kesi imeahirishwa hadi Machi 12, 2019.