Serikali ya Tanzania pamoja na Sudan Kusini zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika kukuza lugha ya Kiswahili ambapo Serikali ya Sudani inatarajia kuanzisha somo hilo katika mitaala yake ya elimu huku Tanzania ikitakiwa kupeleka Walimu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya lugha hiyo.
Makubaliano hayo yaliyofanyika mkoani Dodoma yamesainiwa na Mawaziri wa nchi hizo mbili ambapo kwa upande wa Tanzania ukiwakilishwa na Waziri Joyce Ndalichako na kwa Sudani kusini ukiwakilishwa na Waziri Deng Hoc Yai.
BREAKING: WAZIRI MWAKYEMBE AAGIZA DUDU BAYA KUKAMATWA