Bado gumzo linaendelea kuhusiana na wengi kumkosoa golikipa wa Chelsea Kepa kwa kitendo chake cha kugomea kufanyiwa mabadiliko dakika ya 119 wakati wa mchezo wa fainali ya EFL Cup kati ya Chelsea dhidi ya Man City, kitendo hicho kimekosolewa na walio wengi kiasi cha kufikia kumuunga mkono maamuzi ya Maurizio Sarri.
Baada ya Kepa kutopata nafasi ya kuanza tena kama ilivyokuwa katika michezo mingine na nafasi yake kurithiwa na Caballero, wengi walitaka kujua kulikoni Kepa hachezi tena na kocha alisema kashamsamehe kuwa pale kilichotokea walishindwa tu kuelewana kwa kawaida, hivyo alipomuacha nje katika mchezo dhidi ya Tottenham maswali yalikuwa mengi.
Pedro alipoulizwa kuhusiana na maamuzi ya Sarri kumuacha Kepa vipi hayajawagawanya? “Kumekuwa na maneno mengi sana wiki hii lakini kwetu ni vitu vidogo hivyo lakini ukweli ni kwamba katika vyumba vya kubadilishia nguo tuko pamoja kama timu moja, huwa hatuvipi umuhimu vitu ambavyo havina umuhimu, tumezungumza kila kitu katika vyumba vya kubadilishia nguo niko pamoja na Kepa na kocha pia kila kitu kipo sawa”>>> Pedro
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake