Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa beki wa Simba SC Shomari Kapombea ameanza kuwa vizuri na inaelezwa kuwa atarejea uwanjani hivi karibuni, hiyo ni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti.
Uongozi wa Simba SC umetangaza kuwa baada ya beki huyo kuwa fiti wanamrudisha Afrika Kusini alipokuwa anapatiwa matibabu, Kapombe kabla ya kuanza rasmi mepesi mepesi ya kuanza kurejea uwanjani ameenda Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi wa mwisho.
Kapombe alipata majeraha wakati akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania nchini Afrika Kusini, ambapo ilikuwa imewekwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Lesotho wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019, ambao ulimalizika kwa Taifa Stars kupoteza kwa goli 1-0.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake