Ziwa Ngosi ni moja ya maziwa duniani ambayo yametokana na kulipuka kwa Volcano, Ziwa hilo lipo Mkoani Mbeya nchini Tanzania katika Kijiji cha Mbeye one au Mchangani ni la pili kwa ukubwa Afrika.
Asili ya jina Ngosi linatokana na jina la kabila la Wasafwa linalomaanisha kitu kikubwa na ziwa hilo tangu zamani lilikuwa chini ya himaya ya kabila la Wasafwa katika koo mbili za machifu ikiwemo ya Chifu Mrotwa Mwalingo (akitawala upande wa magharibi) na chifu Mlotwa Mwalupindi (aliyekuwa akitawala upande wa Mashariki).
Ziwa Ngosi lipo usawa wa mita 2600 kutoka usawa wa bahari na limezungukwa na misitu minene ya asili katika safu za milima ya Uporoto na kuna hekari 9,332 ambazo zimetengwa kwajili ya uhifadhi wa eneo hilo.
Ndani ya Ziwa Ngozi kuna visiwa viwili vinavyovutia sana kwa muonekano na inatajwa visiwa hivyo hutumika kwajili ya mazalia ya bata pori na ndege wengine.