Leo March 6, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari mapema ili kukabiliana na majanga ya mafuriko huku akiwataka wakazi wa mabondeni kuhama na hii imekuja baada ya kufuatia tahadhari ya mvua kubwa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa nchini.
RC Makonda amesema ujenzi holela na tabia ya watu kutupa taka kwenye mifereji na mito ndio imekuwa chanzo kikubwa cha mafuriko hivyo amewahimiza wananchi kuacha tabia hiyo huku akitoa siku saba kwa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA kuhakikisha wanaziba viraka katika barabara kwakuwa vimekuwa kero kwa watumiaji wa barabara huku akiwaagiza TANROAD kusafisha miundo mbinu ya mito, mitaro na madaraja yaliyoziba.