Baada ya kuripotiwa kwa tetesi kuwa uongozi wa Real Madrid ya Hispania imefanya mazungumzo na kocha wao wa zamani wa timu hiyo Jose Mourinho, huku ikidaiwa kuwa wako mbioni kumrudisha kocha huyo baada ya timu yao kuyumba na kupoteza muelekeo wa kuwania taji lolote kwa sasa sambamba na kuvuliwa Ubingwa wa UEFA Champions League.
Pamoja na taarifa kusambaa za Real Madrid kuhusishwa kufanya mazungumzo na Jose Mourinho, Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon ameripotiwa kutotaka kocha huyo wa kireno anarudi katika timu hiyo.
“Kiukweli nitakataa wasimrudishe tayari nimeshawaambia kiasi cha uharibifu alichowahi kukifanya hapa, mfumo wake wa uchezaji sio aina ya mfumo ambao unatakiwa Bernabeu, kitu ambacho mashabiki wanataka ni kitu ambacho kama tulichokiona kwa Ajax, umahiri, ujasiri na kasi, Mourinho hawezi kufanya hivyo”>>> Ramon Calderon
Hata hivyo baada ya mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Ajax uliyochezwa Bernabeu na Real Madrid kuaga michuano hiyo baada ya kipigo cha 4-1 (agg 5-3), mashabiki wa Real Madrid mitaanza walirekodiwa wakionekana kuimba jina la kocha wa Kireno Jose Mourinho kama ishara ya kumuhitaji ambaye wamewahi kufanya nae kazi (2010-2013).
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake