Ilivyotokea mpaka TV ya CBS kusimamisha mahojiano kwa muda baada ya Mwimbaji R. Kelly kutekwa na hisia na hasira wakati akikanusha madai ya kuwanyanyasa kingono Wanawake wanne, R. Kelly amedai ni hujuma na wengi hawataki kuuamini ukweli kutoka kwake.
Mwimbaji R. Kelly kwa sasa yupo nje kwa dhamana na amefanya mahojiano yake ya kwanza tangu liibuke sakata la unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, nguli huyo ameshikwa hasira na kumwaga machozi kwenye mahojiano na Gayle King wa CBS.
“Mnaniua na hiki kitu hii sio kuhusu muziki najaribu kutengeneza mahusiano na watoto wangu, na siwezi na hamtaki kuamini ukweli, huu sio ukweli haingii akilini kwanini wanwake wote hawa wazazi wa watoto hao wanasema wataharibu kazi yangu” >>> R.Kelly
VIDEO: WAFANYAKAZI WA CLOUDS WAFUNGUKA WALIVYOPATA AJALI WAKITOKA KUMZIKA RUGE