Tunayo stori kutokea kwa Vijana Chipukizi wa CCM wilaya ya Kinondoni ambapo wamezungmzia ukatili wanaofanyiwa watoto katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni mkoani Njombe.
Akizungumza katika Kongamano Maalum la Watoto wilaya ya Kinondoni, Mwenyekiti wa Chipukizi Tariq Mohammed amesema wameshitushwa na taarifa ya Jeshi la Polisi kwamba Dar es Salaam si salama kwa malezi ya watoto.
“Tumeamua kuandaa kongamano hili ili kupaza sauti kwani taarifa ya mauaji ya watoto wenzetu mkoani Njombe imezidi kutupa hamasa, hivyo tutashirikiana na jeshi la Polisi ili kuzuia uhalifu dhidi ya watoto,”amesema.