Naibu Katibu Mkuu Bara wa CUF aliyetangazwa na Profesa Ibrahimu Lipumba, Magdalena Sakaya amesema CUF ndio ilishawishi kuundwa kwa UKAWA na Mwenyekiti wake ndiye aliyetunga jina hilo la UKAWA.
Akizungumza na waandishi wa habari, Sakaya amesema chama hicho kilikuwa mstari wa mbele kuunda umoja huo kwa lengo la kuwasaidia Watanzania na sio umoja wa chama kimoja.
“Fisadi ambaye tulimchukua CCM na kuikuperusha bendera ya UKAWA leo karudi nyumbani kwao kwahiyo ni ishara kwamba CUF tunahitaji demokrasia imara na sio kuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa, hivyo tutasimamia ukweli na umoja wa haki,“amesema.