Club ya FC Barcelona ya Hispania leo imetangaza rasmi kuwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez watamkosa katika michezo kadhaa kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania LaLiga dhidi ya Real Betis.
FC Barcelona walimtoa Suarez uwanjani dakika za mwisho wakati wa mchezo dhidi ya Real Betis uliyomalizika kwa FC Barcelona kupata ushindi wa magoli 4-1, Jumapili hiyo usiku Luis Suarez alifunga goli lake la 18 la LaLiga.
Kutokana na majeraha aliyoyapata ni wazi FC Barcelona wametangaza kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa siku kati ya 10 had 15, hivyo Suarez pamoja na kuwa alikuwa kaitwa katika kikosi chake cha timu ya taifa ya Uruguay kutokana na kuumia kifundo cha mguu ameondolewa kikosini.
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!