Ni nini kinatakiwa kufanyika?
Mtumiaji aende kwenye vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma anakotaka kuhamia na kuwaeleza kwamba angependa kuhama na namba yake.
Atatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo ni tamko rasmi kwamba anakubali kuwajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma alizokuwa anapata kutoka kwa mtoa
huduma wake wa awali.
Atatakiwa kutoa kitambulisho kinachotambulika na simu ya kiganjani na namba anayotaka kubaki nayo. Iwapo ana salio katika akaunti ya pesa mtandao atashauriwa kutoa pesa kabla
ya kuhama ili kuepuka usumbufu.
Atatakiwa kutuma meseji yenye neno “PORT” kwenda namba ‘15080’ ambayo ni namba maalum ya kuhama. Baada ya haya atapokea meseji kumjulisha kwamba maombi yake yamepokelewa.
Mtoa huduma mpya atampatia laini mpya. Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka, mara nyingi siku hiyo hiyo au, iwapo utachelewa sana, ndani ya saa 48 baada ya kukamilisha utaratibu wa maombi. Wakati huo namba ya mtumiaji itakuwa imeshahamishwa kwa mtoa huduma wake mpya na laini yake ya awali haitatumika tena.
Ikifikia hapo, mtumiaji anatakiwa kuweka laini mpya aliyopewa na mtoa huduma wake mpya kwenye simu anayotaka kutumia. Mchakato umekamilika.
Iwapo mtumiaji hana uhakika wa nini cha kufanya, anaweza kwenda kwa mtoa huduma wake mpya au wakala wake kwa msaada