Moja kati ya habari kubwa iliyokuwa inaendelea katika mitandao ya kijamii wakati kukiendelea na uhamasishaji wa mashabiki wa timu ya taifa ya Tanzania kuwa waende uwanjani katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda wakiwa wamevaa jezi kuisapoti timu yao.
Jezi rasmi za timu ya taifa ya Tanzania zilikuwa hazipatikani mtaani huku mawakala wa UhlSports ambao ndio watengenezaji wa jezi za Taifa Stars kusema kuwa hawana mkataba wa kuuza jezi hizo zaidi ya kupewa jukumu la kuitengenezea Taifa Stars jezi za mechi katika kila mchezo na sio kuuza.
Hivyo mashabiki wengi walienda uwanjani na jezi feki na zisizoiletea chochote TFF, kwani zilitengenezwa na kuuzwa na watu wasiokuwa na makubaliano rasmi na TFF, Rais wa TFF Wallace Karia akihojiwa na Clouds 360 ya Clouds TV ameizungumzia ishu hiyo.
“Unapoingia kwenye uongozi kuna mambo ya kuyafanyia kazi nimeshalifanyia kazi, ile nembo ya TFF tumeingia mkataba na kampuni ya Umbro wanaotengenza jezi za kimataifa zitauzwa kwa Tshs 35000 pia wataingia mkataba na mfanyabiashara atakayeuza jezi”>>> Wallace Karia
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS