Inaripotiwa kuwa Mwigizaji wa Empire Jussie Smollett amefutiwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili siku ya March 26,2019 ambapo alishtakiwa kwa makosa 16 ya kuidanganya Polisi na kudaiwa kupanga shambulio la kupigwa na watu wawili wasiojulikana kwa madai ya ubaguzi wa rangi na tuhuna za ushoga.
Inaelezwa kuwa Jussie Smollet alituma barua ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa mapenzi ya jinsia moja kwa kampuni ya Fox studio anayofanya nayo kazi siku moja kabla ya shambulio huku ikiripotiwa kuwa Jussie alijisalimisha mikononi mwa Polisi siku ya Feb 21,2019 ili kusikiliza mashtaka yake ya kuwadanganya Polisi kuhusu kutekwa.
Jussie Smollet alikana mashtaka yote na kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 233 za Kitanzania.
ULIPITWA NA SHAVU LILILOTOLEWA KWA VIJANA WA KITANZANIA KWENDA HOLLYWOOD KUPITIA MASTER TANZANIA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA