Club ya Chelsea ya England imeripotiwa kuwa katika mipango ya kumpeleka kwa mwanasaikolojia staa wake Callum Hudson-Odoi kutokana na mchezaji huyo kukumbwa na changamoto za ubaguzi wa rangi akiwa katika club yake na timu yake ya taifa ya England kote hakuna unafuu.
Callum mwenye umri wa miaka 18 atafanyiwa ushauri nasaha (counselling) baada ya kujikuta katika wakati mguu wa kubaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yake akiwa katika timu yake ya Chelsea na England timu ya taifa kwa nyakati mbili tofauti, Callum kwa mujibu wa dailymail atafanyiwa ushauri nasaha (counselling) kwa muda wa wiki mbili.
Staa huyo kinda wa Chelsea alikutana na tukio la kibaguzi akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya England Raheem Sterling na Danny Rose wakiwa katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Euro 2020 dhidi ya Montenegro mchezo ambao ulimalizika kwa England kushinda 5-1.
Kutokana na kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki wao kuwaita wachezaji wa England kama nyani, Montenegro tayari wamefunguliwa shitaka na UEFA na litasikilizwa May 16 na kama watakutwa na hatia ya kutenda kosa hilo basi adhabu yao ya chini kabisa inaweza kufungiwa kuingiza idadi ya mashabiki wengi uwanjani.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars