Tanzania ina hazina kubwa sana ya watu wenye kupenda michezo na kwa kiasi kikubwa mchango wa waandaaji wa mashindano ya michezo kama mchezo wa riadha ni muhimu. Kwa kutambua hili ndio maana tumeanzisha Selous Marathon ambazo kwa mwaka huu wa kwanza zitafanyika Morogoro August 28 2019 na kilele kitakuwa August 25 2019
Selous Marathon kwa mwaka huu itashirishikisha mbio za kilomita 21, kilomita 10, kilomita 5 yaani mbio za furaha na pia kilomita 2.5 kwa ajili ya watoto, kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo Rehema Jonas Mwendo ametangaza rasmi uzinduzi wa Mbio hizi.
Mbele ya waandishi wa habari muwakilisha Mkurugenzi wa Michezo Neema Msita aliipongeza kamati ya maandalizi kwa mwanzo mzuri na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia na ameitaka jamii kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizi na kutumia michezo kwa ajili ya kuboresha Afya hivyo aliihasa jamii kupenda michezo.
Aidha waaandaaji wameishukuru Wizara ya michezo kwa kutoa kibali na kusajili mbio hizo, pia wameshukuru RT kwa miongozo na wamehaidi kuendelea kutumia ushauri na mawazo kwa miezi mitano Zaidi ijayo,Shukran zingine ni kwa katibu wa Riadha wa mkoa wa Morogoro Mr Kibukila na Mjumbe wa Kamati ya ufundi RT Mr Kalyale.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars