Mkurugenzi wa Mipango TAKUKURU, Kulthum Mansoor, ambaye Machi 28, 2019, alitajwa na Rais Magufuli kwa tuhuma za kuwadhulumu viwanja, baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TAKUKURU amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay.
Imeelezwa kwamba wakati jana Rais Magufuli alipokuwa anamzungumzia kigogo huyo, uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ulikuwa umekamilika
March 28, 2019 Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola alisema anashangazwa kwa Taasisi hiyo kutomchukulia hatua yeyote Mkurugenzi huyo.
KAULI YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU RIPOTI YA TAKUKURU “WANAWAKE NI WAAMINIFU”