Leo March 29. 2019 TAKUKURU imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliyekua Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Kulthum Mansoor akidaiwa kuwauzia viwanja feki wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Kulthum alitajwa na Rais Magufuli baada ya kumuapisha Balozi wa Cuba,Valentino Mlowola pamoja na kupokea ripoti yaTAKUKURU alisema anashangazwa kuona TAKUKURU bado hawajamchukulia hatua mtuhumiwa hiyo mpaka sasa.
Magufuli alisema kuna Mkurugenzi mmoja pale TAKUKURU ambaye amewauzia wenzake viwanja hewa vyenye thamani ya Bilioni 1 na Milioni 400 lakini mpaka sasa hajapelekwa mahakamani.
Hata hivyo Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema kuwa, wakati rais Magufuli anamtaja, upelelezi ilikua tayari umekamilika.
LIVE: BOSI TAKUKURU ALIETAJWA NA JPM | ALITAPELI BILIONI 1 NA MILIONI 600 AMEKAMATWA