Siku moja imepita toka club ya Man United impe mkataba wa kudumu aliyekuwa kocha wao wa muda wa club hiyo Ole Gunnar Solskjaer, Man United imeamua kumpa mkataba wa miaka mitatu baada ya kujiridhisha kuwa Solskjaer anastahili kuendelea na kuifundisha Man United.
Ole Gunnar Solskjaer amepewa mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha timu hiyo, awali alikuwa amepewa mkataba wa muda mfupi kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu aliyekuwa amechaguliwa kumrith Jose Mourinho aliyefutwa kazi na Man United December 2018.
Ole Gunnar ameongea kwa mara ya kwanza baada ya kusaini mkataba huo “Hii imekuwa ndoto yangu ya muda wote, nitakuwa yule yule kama nilivyokuwa siku zote na najua matarajio ya klabu, utamaduni wa club na historia ya club, bila shaka najua nitafanya vizuri na nitafanikiwa na kuinua mataji”>>>Ole Gunnar Solskjaer
Uongozi wa Man United umefikia hatua ya kumuamini Ole Gunnar Solskjaer na kumpa mkataba wa miaka mitatu, baada ya kuiongoza Man United katika michezo 19, wakishinda 14, sare michezo miwili na wamepoteza michezo mitatu, huku Solskjaer akiweka rekodi kuwa kocha wa kwanza wa Man United katika historia kushinda michezo 9 ya ugenini mfululizo.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars