Game inayozikutanisha timu za Zamalek na Al Ahly za nchini Misri ni moja kati ya game zinazoteka hisia za mashabiki wengi wa soka nchini Misri, kuelekea mchezo huo mara nyingi kunakuwa na presha kubwa kwa mashabiki wa pande mbili na wakati mwingine zinaweza kuzuka vurugu za mashabiki.
Kesho March 30 2019 utachezwa mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri ambao utahusisha timu hizo, kuelekea mchezo huo zimetangazwa taarifa ambazo sio za kawaida sana kwa mashabiki, mchezo huo Al Ahly ndio atakuwa mwenyeji kumkaribisha Zamalek katika uwanja wa Borg-al-Arab unaochukua mashabiki 86,000.
Kwa mujibu wa chama cha soka Misri EFA kimetangaza kuwa baada ya kukaa kikao na watu wa usalama na kujadiliana, wameridhia kuwa mchezo huo utachezwa na kuruhusiwa kuingia mashabiki 30 tu uwanjanji, 15 kwa kila timu licha ya uwanja kuwa na uwezo wa kuchukua watu 86000.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars