Leo April 1, 2019 Maalim Seif Sharif Hamad amehojiwa katika Kipindi cha Clouds 360 nakujibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho Babie Kabae na Hassan Ngoma. Nimekusogezea mambo aliyozungumza Maalim Seif japo kwa ufupi.
“Si kweli kwamba nimetoka CUF kwa sababu nilikataa kubadilika kimkakati, kama kubadilisha strategy (mkakati) ni kushirikiana na CCM, mimi sikuwa tayari na siko tayari” Maalim Seif#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ModVpgS1ZZ
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Nawapeni pole sana kwa kuondokewa na kijana wenu Ruge, alikuwa mtu wa watu na hilo limethibitishwa na msiba wake ulivyozizima nchi nzima, poleni sana” Maalim Seif
Via Clouds360#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/zrR4mTy6dy
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Tulifungua kesi nyingi Mahakamani ili kutafuta haki, lakini dola ilikuwa imedhamiria kumpa Chama Lipumba, tukaanza kujipanga kwa lolote” Maalim Seif
Via Clouds360#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/F2aAGoI5zD
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Uamuzi wa kuhama CUF kwenda ACT Wazalendo haukuwa uamuzi wa siku moja, ulikuwa uamuzi tulioufanya kwa umakini baada ya kuona hatari ya kunyang’anywa chama” Maalim Seif
Via Clouds360#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/S9kqaIEqii
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Kama muda muafaka ukifika na mkinikaribisha nitakuja hapa kutangaza uamuzi wangu wa kugombea au kutogombea Urais, muunganiko wa Viongozi waliokuwa wa ACT na sisi tuliotoka CUF utaleta mabadiliko makubwa, tupeni muda” Maalim Seif
MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/U2xgpMc0D2
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Bado sijarudisha kadi ya CUF, tumekubaliana sote, tutakusanya kila kitu cha CUF tulichokuwanacho, kadi, bendera, Katiba kisha tutampa Kiongozi wa Chama chetu ACT Wazalendo apeleke kwa Msajili halafu Msajili mwenyewe atajua avifanyie nini” Maalim Seif#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/AvBK25Tn40
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Hili jambo halikutokea ghafla ingekuwa hivyo lingeniuma sana lakini tuliona dola ina nia ya kumpa Lipumba chama cha CUF, tuliamua kujipanga, ukiwa na mke ukiishi naye miaka mingi, mmezoeana nae akiondoka, utaumia lakini mwisho wa siku utazoea” Maalim Seif#MillardAyoPDATES pic.twitter.com/1TziQE8knA
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Niko na afya njema tena baada ya kuhama chama, afya yangu imeimarika” Maalim Seif
Via Clouds360#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/dETGrkX85z
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Kuhama kwangu sidhani kama tunavuruga wanachama wenyewe walishachoka na mgogoro huu, waliumia nilivyohama lakini baada ya masaa matatu tu baada ya kuhamia ACT Wazalendo walifarijika na mliona walivyonifuata, tunashusha Tanga, tunapandisha Tanga” Maalim Seif#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/u83fh7tSIz
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Majengo ya CUF yaliyokuwa mali ya chama ni Kilimahewa, Buguruni na mengine yaliyobaki yalikuwa ni majengo ya wanachama wa CUF ambao waliikodisha CUF sasa mtu aliyekodisha na kaamua kuhama chama asipake rangi ya Chama anachotaka? ” Maalim Seif#MillardAyoPDATES pic.twitter.com/0GCL5jHCbg
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
“Tumekwenda ACT sio kutafuta vyeo, tumekwenda kuongeza nguvu kwenye upinzani, wakitutunuku vyeo tunavipokea ” Maalim Seif#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/qUSCfG014q
— millardayo (@millardayo) April 1, 2019
Watu watatu majambazi raia wa Burundi wameuawa Kigoma