Jumamosi ya April 13 2019 itakuwa ni siku ya game ya marudiano ya robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe mjini Lubumbashi Congo DR, mchezo huo utachezwa kuamua nani anatinga nusu fainali CAF Champions League kati ya Simba na TP Mazembe baada ya game ya kwanza Dar es Salaam kumalizika 0-0.
Kuelekea mchezo huo shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza kubadili waamuzi wa mchezo huo kwa sababu walizodai za kiufundi, awali mchezo huo ulikuwa uchezeshwe na waamuzi kutokea Ethiopia na Kenya lakini CAF limewatangaza waamuzi wapya kutokea Zambia na Eritrea.
CAF limewatangaza Janny Sikazwe raia wa Zambia ndio kuwa muamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi ni Berhe O’Michael kutoka Eritrea, Romeo Kasengele kutoka Zambia na Fourth Official akiwa ni Audrick Nkole kutoka Zambia sababu kuu zilizotajwa na CAF ni ufundi.
Kama humfahamu vizuri Janny Sikazwe amewahi kuchezesha game za FIFA Club World Cup 2016 iliyowakutanisha Real Madrid dhidi ya Kashima Antlers, Sikazwe pia alikuwa muamuzi wa baadhi ya michezo ya fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika nchini Urusi ukiwemo mchezo wa Belgium dhidi ya Panama.
“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC