Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwimbaji mkongwe wa miondoko ya RnB R.Kelly alitangaza kufanya tamasha lake la kwanza siku ya Jumapili April 7,2019 nchini Marekani tangu aachiwe kwa dhamana February 26,2019 na kuelezwa kuwa R.Kelly hakufanikiwa kutumbuiza.
Inaripotiwa kuwa kutokana na idadi ya mashabiki waliohudhuria show hiyo kuwa ndogo, ukumbi wa Dirty South uliamua kushusha bei za tiketi ili mradi wapate watu huku baadhi ya mashabiki walifanikiwa kupata nafasi ya kupiga picha (selfies) na R.Kelly na kuonyesha kufurahia kumuona japo show hiyo ilibuma.
Baada ya tukio hilo wengi wametafsiri kuwa R. Kelly ameanza kupoteza mashabiki kutokana na muimbaji huyo kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo ambapo baadhi yao walitoa ushuhuda kupitia makala yake ya ‘Surviving R.Kelly’.
VIDEO: SABABU YA KIFO CHA JESSIE CHATAJWA/ MAZISHI MOROGORO